

Lugha Nyingine
医保“谈判目录”出炉 11家上市公司重磅新药入围
![]() |
Njia ya wakimbiaji iliyoinuliwa na uwanja wa soka kwenye Kituo cha Viwanja vya Michezo cha Xicun. (People's Daily Online /Gu Yutong) |
Michezo ya Dunia 2025 itafanyika mwezi huu mjini Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tukio hilo la michezo ya kimataifa kufanyika China Bara. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo umekuwa ukifungamanisha kikamilifu mazoezi ya utimamu wa mwili na maendeleo ya mji kwa kuunda nafasi maalumu za umma kama vile Kituo cha Viwanja vya Michezo cha Xicun.
Kikiwa kilisanifiwa na msanifu aliyetunukiwa Tuzo ya Usanifu Majengo ya Pritzker Liu Jiakun, Kituo hicho cha Viwanja vya Michezo cha Xicun kimekuwa kikivutia macho ya watu wengi tangu kilipokamilika mwaka 2014, hasa kwa njia yake ya wakimbiaji iliyoinuliwa yenye urefu wa kilomita 1.6. Ikianzia kwenye ardhi, njia hiyo inazunguka kwenda juu hadi kwenye paa la ghorofa ya tano, ambako watembeleaji wanaweza kufanya mazoezi ya kukimbia, kutembea, au kufurahia kutazama mandhari kamili ya mji.
Kituo hicho pia kina uwanja wa soka wa timu za wachezaji saba kila upande na uwanja sanifu wa mpira wa kikapu, ikikifanya kuwa kituo maarufu kwa wakazi wenyeji.
Kikiwa ni sehemu muhimu ya kazi ya miundombinu ya mji na alama ya utamaduni wa michezo wa Chengdu, Kituo hicho cha Xicun kimeshakuwa mwenyeji wa matukio mbalimbali ya michezo ya ngazi za kitaifa, kimkoa, na kimiji. Kinasimama leo kama jukwaa muhimu la kuhimiza mazoezi ya utimamu wa mwili kwa umma na kuonesha uzuri wa hali motomoto wa mji huo.
Wakati Michezo ya Dunia inapokaribia, Kituo cha Viwanja vya Michezo cha Xicun kipo tayari kukaribisha watembeleaji kutoka duniani kote.
Miujiza ya Wanyamapori: Kutoka Mbuga Tambarare za Afrika hadi Uwanda wa Juu wa Qinghai -Tibet, China
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma